Saturday, January 20, 2018

SIMBA WAFANYA MAZOEZI NTUNGAMO BUKOBA, TAYARI KWA MCHEZO WAO WA VPL NA KAGERA SUGAR KAITABA


Na Faustine Ruta, Bukoba
KLABU ya Simba mapema jana imefanya mazoezi yake kwenye uwanja wa Ntungamo Bukoba kujiweka tayari na mchezo wao wa Ligi kuu dhidi ya Timu wenyeji Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.Simba wanajifua ikiwa ni siku mbili tu wameifanyia kitu mbaya Timu ya Singida United bao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mshambuliaji wake hatari wa kuzifumania nyavu, Mganda Emmanuel Okwi akifunga mabao mawili.
Ushindi huo dhidi ya Singida United umeifanya Simba SC ifikishe pointi 29, baada ya kucheza mechi 13, ikiwazidi pointi saba mabingwa watetezi, Yanga SC na pointi mbili Azam FC wenye 27 katika nafasi ya pili, wakati Mtibwa Sugar sasa ni ya tatu kwa pointi zae 24 baada ya timu zote kucheza mechi 13.
Wekundu wa Msimbazi pia wanataka alama 3 muhimu pia zipatikane kwenye Uwanja wa Kaitaba watakapo pambana na wenyeji Kagera Sugar mjini Bukoba.