Saturday, January 20, 2018

SIMBA WAINGIA BUKOBA MAPEMA, TAYARI KWA MCHEZO JUMATATU NA KAGERA SUGAR

Mapema asubuhi ya leo kikosi cha klabu ya soka ya Simba kimetua mkoani Kagera kwa ajili ya kucheza mechi yao ya ligi kuu Tanzania Bara na Kagera Sugar.
Kikosi cha Simba kilivyowasili uwanja wa ndege wa Kagera
Simba waliondoka alfajiri kwa ndege huku ikiwa na wachezaji wake muhimu ambao jana waliiangamiza Singida United kwa mabao 4-0.
Simba ambao wanaongoza Ligi hiyo inatarajiwa kucheza na Kagera Sugar Jumatatu ya wiki ijayo ya January 22 katika uwanja wa Kaitaba.Mashabiki mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kuwapokea katika Uwanja wa Ndege mjini hapa Bukoba.

Wachezaji wa Simba mara baada ya kushuka kwenye Ndege

Wakati kikosi kikiwasili mjini Bukoba, Jijini Dar es Salaam Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amemtambulisha kocha mpya, Mfaransa, Pierre Lechantre pamoja na Msaidizi wake, kocha wa mazoezi ya viungo, Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi.Katika hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa Kivukoni, hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam, Abdallah alimsainisha mkataba Lechantre, ambao hata hivyo hawakusema wa muda gani.Abdallah amesema kwamba Mfaransa huyo anaingia Simba SC kwa ajili ya programu maalumu ya kuinoa timu ya wakubwa na wadogo.Lechantre ambaye ataanza kazi timu itakaporejea kutoka Bukoba, amesema anaomba apewe angalau miezi minne ili wana Simba waanze kufurahia kazi yake.

Mabeki, Mganda Juuko Murshid na mzawaMohammed Hussein 'Tshabalala' wakiwakwenye ndege leo
Pierre Lechantre aliyezaliwa Aprili 2, mwaka 1950 mjini Lille, Nord, Ufaransa ni kocha aliyeipa Cameroon ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2000 na kabla ya kuanza kufundisha alikuwa mchezani pia.Aprili 27 mwaka 2012, Lechantre alitambulishwa kuwa kocha Mkuu wa Senegal, lakini akashindwa kufikia makubaliano ya mwisho na Shirikisho la Soka la nchi hiyo.Akiwa mchezaji katika nafasi ya ushambuliaji, Lechantre amechezea klabu za Paris FC (1986–1989), Red Star 93 (1983–1986), Stade de Reims (1981–1983), Olympique de Marseille (1980–81), RC Lens (1979–80), Stade Lavallois (1976–1979), AS Monaco (1975–76), FC Sochaux (1970–1975) na Lille OSC (1964–1970).


Mashabiki wa Simba wakiwa tayari kwa kuwapokea SimbaJezi ya Mnyama simba