Sunday, January 21, 2018

SIMBA WAJIFUA KAITABA, KESHO KUPAMBANA NA WENYEJI KAGERA SUGAR.Na Faustine Ruta, Bukoba 

Kikosi cha Timu ya Simba kimefanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, yakiwa ni maandalizi ya kukabiliana na kikosi cha Timu ya Kagera shugar hapo kesho jioni.
Kikosi hicho ambacho kinaongozwa na Kocha Masoud Djuma ambacho kilitua katika ardhi ya Kagera siku ya Ijumaa kimefanya mazoezi ya mwisho katika dimba la Kaitaba, huku kocha wa kikosi hicho akisema mechi yao na Kagera sugar itakayopigwa hapo kesho inahitaji nidhamu ya hali ya juu ili kuweza kuibuka kidedea.
Nacho Kikosi cha timu ya kagera sugar kilifanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jana asubuhi kabla ya kukutana na wekundu wa msimbazi, mchezo utakao chezwa siku ya jumatatu katika dimba la Kaitamba.
Kagera sugar wanakutana na Simba wakiwa na taadhali kubwa baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Njombe mji huku Simba wakiwaadabisha matajiri wa Arizeti Singida United kwa mabao 4-0 wiki hii.
Katika mazoezi ya hayo kocha wa timu ya Kagera Sugar  Mecky Meckime amezungumzia maandalizi ya mchezo huo na kueleza kuwa kikosi chake kiko imara licha ya kutokuwa na matokeo mazuri tangu Ligi hii ianze msimu 2017/2018.

Emmanuel Okwi akiwa kati walipokuwa wanafanya mazoezi hii leo asubuhi katika Uwanja wa Kaitaba.
Mshambuliaji Laudit Mavugo raia wa Burudi nae alikuwepo katika mazoezi hayo.
Emmanuel Okwi
Wakati huo huo nao waamuzi nao walikuwepo wanafanya mazoezi
Walinda mlango wa Timu ya Simba Sc(kulia) ni Aishi Manula ambaye amejifunga kwa miaka miwili Simba. (kushoto) ni Said Mohammed Nduda
Wakijiuliza kuhusu mechi ya Kesho Kaitaba
Kocha wa Simba Masoud Djuma nae kapasha na Wachezaji wake
(kulia) ni Shabani Kapombe
Kocha wa Simba Masoud Djuma(kushoto)
Mavugo


kushoto ni Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya

Kesho Hapatoshi!!
Kocha wa Simba Masoud Djuma akiteta jambo na mwandishi(hayupo pichani) kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba hii leo wakati wa Mazoezi ya Mwisho kabla ya kukutana na Timu wenyeji Kagera Sugar.
(Kulia) ni Willy O. Ruta akiwa na Kiongozi wa Timu ya Simba
Makipa wakipimana

Taswira kamili za Mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Kaitaba