Sunday, January 14, 2018

TOTTENHAM YASHINDA KANE AKIVUNJA REKODI YA UFUNGAJI MAGOLI YA KLABU, WAIFUNGA EVERTON BAO 4-0, ROONEY ADUWAA!!

Meneja wa Tottenham Mauricio Ponchettino anaunga mkono Harry Kane kuvunja rekodi ya ufungaji ya klabu hiyo mara baada ya kufunga magoli mawili katika ushindi mwepesi wa magoli 4-0 dhidi ya Everton.
Harry Kane alifunga magoli hayo mawili karibu na lango akimalizi pasi za Son Heung-min na Eric Dier na kufikisha idadi ya magoli 98 katika Ligi Kuu ya Uingereza akimzidi Teddy Sheringham kwa goli moja aliyoifungia klabu hiyo.
Katika mchezo huo Son aliyekuwa kwenye ubora wake alifungua mvua ya magoli akiunganisha wavuni krosi ya Serge Aurier. Tottenham ilipata goli lake la nne kupitia kwa Christian Eriksen akinasa pasi ya kisigino ya Dele Alli.
Mshambuliaji Harry Kane akifunga moja ya magoli yake mawili aliyofunga jana.
Mshambuliaji raia wa Korea Kusini Son Heung-min akiifungia Tottenham goli la kwanza.