Thursday, January 4, 2018

TOTTENHAM YASHINDA NA KUIPIKU ARSENAL KATIKA MSIMAMO WA LIGI

Timu ya Tottenham imeipiku Arsenal na kupanda katika nafasi ya tano ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuifunga timu iliyomkiani ya Swansea City kwa magoli mawili kwa bila katika dimba la Liberty.
Ikicheza huku nyota wao Harry Kane akianzia benchi, alikuwa Fernando Llorente aliyeipatia Tottenham goli la kwanza kwa mpira wa kichwa akiifunga timu yake ya zamani huku akionekana kama ameotea.
Swansea ilishindwa kumudu mashambulizi ya Spurs na katika dakika ya 89, Kane alitoa pande kwa Dele Alli ambaye shuti lake la kwanza liliokolewa na Lukasz Fabianski kabla ya kuukuta mpira na kutumbukiza kimiani.
Fernando Llorente akifunga goli la kwanza la Tottehnam kwa mpira wa kichwa
Dele Alli akishangilia goli alilofunga akiwa na Harry Kane ambaye ndiye aliyempasia mpira