Tuesday, January 16, 2018

UHAMISHO 2018: HAKUNA MAKUBALIANO YA MKHITARY KWENDA ARSENAL MPAKA SASA!

Hakuna makubaliano yaliofikiwa kwa mshambuliaji wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan kujiunga na Arsenal ili kuwa mbadala wa Alexis Sanchez, kulingana na duru iliokaribu na Mkhitaryan.
Inaaminika kwamba Sanchez ameingia katika makubaliano ya kibinafsi na United.
Lakini Man United na Arsenal haziwezi kuafikiana makubaliano yoyote bila Mkhitaryan kwenda Arsenal.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anaaminika kutathmini mpango huo na hana haraka ya kutoa uamuzi wa mwisho.

United iliipiku Arsenal katika kumsajili Mkhitaryan kutoka klabu ya Borussia Dortmund kwa dau la £26m mnamo mwezi Julai 2016.

Hataki kutoka Old Trafford kwa lolote lile lakini ana wazo tofauti na lile la Jose Mourinho na hatua hiyo imeongeza uwezekano wa yeye kuondoka.
Inadaiwa kuna sababu nyengine mbadala katika meza na hilo haliondoi dhamira yake ya kutaka kusalia Man United ambapo amepewa kandarasi ya hadi 2020.
Pia inaaminika kwamba Dortmund imakataa kuwasilisha ombi la kutaka kumsajili tena Mkhitaryan.

Timu hiyo ya Ujerumani ilimuulizia Mkhitaryan kabla ya dirisha la uhamisho kufunguliwa lakini wakahisi kwamba dau la uhamisho wake ni la juu mno.
Huku wakijulikana kwa kuwasiliji upya wachezaji kadhaa ambao walikuwa wameondoka klabu hiyo akiwemo mchezaji wa zamani wa United Shinji Kagawa, inaaminika kwamba hawana hamu ya kumrudisha tena Mkhitaryan.
Dortmund vilevile haijapata ombi lolote kutoka kwa Arsenal la kumnunua mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.

The Gunners wanadaiwa kwamba wana hamu kubwa ya kumsajili Aubameyang ambaye hakuchezeshwa wikendi iliopita kutokana na maswala ya utovu wa nidhamu.