Sunday, January 21, 2018

YANGA YAIFUNGA RUVU SHOOTING BAO 1-0, MFUNGAJI NNI PIUS BUSWITA!

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Bao la Yanga lilifungwa katika muda wa nyongeza wa kipindi cha kwanza na Pius Buswita kwa kichwa, akiunganisha wavuni mpira uliopigwa na Ibrahim ajib.
Sekunde chache kabla ya bao hilo, Ruvu Shooting walikosa bao la wazi katika dakika ya 45 baada ya Abdulrahman Mussa kupiga shuti nje wakati kipa wa Yanga, Youthe Rostand akiwa hayupo golini.
Ruvu Shooting walikosa tena bao baada ya Issa Kanduru kushindwa kufunga katika dakika ya 62 baada ya kufanikiwa kumpiga chenga kipa wa Yanga, Rostand kabla ya kufunga beki Hassan Kessy kuokoa.

Kwa ushindi huo, Yanga sasa imefikisha pointi 25 baada ya mechi 14, huku jahazi la Ruvu Shooting likiendelea kuzama ikiwa na pointi 11 mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo yenye timu 16.

Kwa pointi hizo, Yanga imeitoa Mtibwa Sugar katika nafasi ya tatu, licha ya timu hizo kuwa na pointi sawa, lakini mabingwa hao watetezi wana uwiano mzuri wa mabao.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Mwadui FC ambayo wiki iliyopita ilitoka sare na Yanga kwenye Uwanja wa Uhuru, imetoka sare na Ndanda katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.