Friday, February 16, 2018

EUROPA LEAGUE: ARSENE WENGER AIPONGEZA ARSENAL BAADA YA KUIBUKA NA USHINDI SWEDENIWA BAO 3-0


Arsene Wenger amekipongeza kikosi chake cha Arsenal kwa namna walivyomudu mazingira mageni na kuifunga Ostersunds FK ya Swedeni kwa magoli 3-0 katika mchezo wa Ligi ya Europa.
Mchezo huo ulichezwa kwenye hali ya hewa ya nyuzi joto -4 katika dimba la 4G la plastiki la
Jamtkraft Arena, lakini wageni Arsenal waliweza kupata ushindi mzuri huku beki wa kushoto Nacho Monreal akifunga goli la kwanza.
Beki wa kati wa Ostersunds FK Sotirios Papagiannopoulos alijifunga goli akijaribu kuzuia krosi ya Henrikh Mkhitaryan, baada ya hapo Ostersunds ilijaribu kuimarika lakini Mesut Ozil, akaifungia Arsenal goli la tatu.


Nacho Monreal akiifungia Arsenal goli la kwanza katika mchezo huo

Mpira wa krosi ya Henrikh Mkhitaryan ukitumbukia kimiani baada ya beki
Sotirios Papagiannopoulos kujifunga