Saturday, February 17, 2018

FA CUP FULL TIME: CHELSEA 4-0 HULL CITY


Olivier Giroud na Willian wameisaidia Chelsea kuichakaza Hull City na kutinga robo fainali ya kombe la FA, kwa kuichakaza kwa magoli 4-0.
Willian alikuwa katika kiwango bora katika muda wote ambapo alifunga goli la kwanza kwa shuti la mpira wa kuzungusha akiwa eneo la nje ya boksi.
Pedro alifunga goli la pili akiunganisha pasi ya iliyopigwa na Cesc Fabregas, kisha Willian akafunga goli lake la pili na Giroud akafunga la nne.


Mbrazil Willian akiwa ameachia shuti kali lililozaa goli lake la pili

Olivier Giroud akijitambulisha vyema Chelsea kwa kuifungia goli timu yake hiyo mpya