Saturday, February 17, 2018

FA CUP: RIYAD MAHREZ AISAIDIA LEICESTER KUSHINDA BAO 1-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI


Timu ya Leicester City imeweka kando sakata la uhamisho wa Riyad Mahrez baada ya mchezaji huyo raia wa Algeria kuisaidia kutinga robo fainali ya Kombe la FA, kocha wa timu hiyo Claude Puel amesema.
Mahrez, ambaye alirejea kikosini baada ya kukosekana mazoezini kwa siku 10, baada ya pendekezo la kuhamia Manchester City kugonga mwamba, alimtengenezea nafasi ya kufunga mshambuliaji Jamie Vardy na kufanya matokeo kuwa 1-0 dhidi ya Sheffield United.


Mpira uliopigwa na Jamie Vardy ukitinga wavuni na kuandika goli pekee katika mchezo huo

Jamie Vardy akifunga goli ambalo hata hivyo lilikataliwa na refa msadizi katika mchezo huo