Sunday, February 4, 2018

FULL TIME: BURNLEY 1-1 MANCHESTER CITY


Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amegoma kumlaumu Raheem Sterling kwa kuchangia kuinyima ushindi City dhidi ya Burnley baada ya mchezaji huyo kupoteza nafasi nzuri ya kufunga.
Manchester City ikiwa inaongoza kwa goli 1-0 zikiwa zimebakia dakika 20 mchezo kumalizika, Sterling alishindwa kuongeza goli la pili katika umbali wa yadi sita baada ya kukutana na krosi ya Kyle Walker.

Kitendo hicho kilimfanya azomewe na mashabiki wa timu yake na kisha kulazimika Sterling kutolewa nje kupumzika na baadaye Johann Berg Gudmundsson alipoisawazishia Burnley zikiwa zimebakia dakika nane mpira kuisha.


Mchezaji Raheem Starling akipoteza kizembe nafasi nzuri ya kuongeza goli la pili

Mchezaji Johann Berg Gudmundsson akishangilia baada ya kuisawazishia Burnley