Saturday, February 17, 2018

FULL TIME VPL: KAGERA SUGAR 1 vs 1 SINGIDA UNITED, MH. MWIGULU NCHEMBA ASHUHUDIA KIPUTE HICHO KAITABA.

Timu ya Kagera Sugar ndio ilipata bao ikiwa ya kwanza kupitia kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Singida United kuunawa ndani ya 18, Mkwaju uliopigwa na Beki wa Kagera Sugar Mohammed Fakhi. Kipindi cha pili Singida United walirudi na nguvu na kufanikiwa kuiteka ngome ya Kagera Sugar na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha mapema kipindi cha pili.

Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar kilichoanza
Kikosi cha Timu ya Singida United kilichoanza dhidi ya Timu ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba leo.
Picha na Faustine Ruta, BukobaWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) (katikati) akishuhudia mtanange huo kwenye Uwanja wa Kaitaba. Kagera Sugar wametoshana nguvu na Singida United. Picha na Faustine Ruta, BukobaKulia ni Wachezaji wa Kagera Sugar wakimpongeza Mohamed Fakhi baada ya kufanikiwa kuifungia bao kwa mkwaju wa Penati Kagera Sugar kipindi cha kwanza.Kipa wa Singida United hakuna kitu!! Kagera Sugar 1-0 Singida United katika kipindi cha kwanza cha dakika 45.

Batambuze akiwa chini ya Ulinzi.


Kocha wa Singida United, Hans Pluijm akiwa hana hamu baada ya kwenda mapumziko akiwa nyuma ya bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar. Picha na Faustine Ruta, Bukoba

Baadae kipindi cha pili Kocha wa Singida United, Hans Pluijm aliwapa mbinu Singida United.