Tuesday, February 6, 2018

FULL TIME: WATFORD 4 vs 1 CHELSEA, ROBERTO PEREYRA, GERARD DEULOFEU ANA DARYL JANMAAT WAZIONA NYAVU ZA BLUES, CONTE ALIA NA WACHEZAJI WAKE. KIBARUA CHAKE KIKAANGONI!!!


Wachezaji wa Watford Roberto Pereyra, Gerard Deulofeu na Daryl Janmaat wote waliziona nyavu za Chelsea Jumatatu usiku kwenye Ligi kuu ya EPL -England. Chelsea waliumaliza Mtu kumi uwanjani baada ya Bakayoko kutolewa kwa kadi nyekundu uwanjani na ndipo mambo yaliwageukia Chelsea na kufungwa magoli mengi dakika za mwishoni mwa mchezo na kumaliza 4-1. Wachambuzi walimhoji kocha Conte kuhusu kibarua chake na yeye waziwazi alisema kuwa aliwaonya wachezaji wake kucheza mchezo mzuri lakini kipingo hicho kinamweka pabaya Kocha huyo Conte. Huku kukiwa na tetesi kwamba alikuwa amepewa muda kubadilisha matokeo katika mtanange huo.Gerard Deulofeu na Javi Gracia wakishangilia baada ya bao huku wakiwa wanamwongezea machngu kocha Chelsea  Antonio Conte
Daryl Janmaat alifanya  2-1 muda mfupi baada ya Chelsea kusawazisha
Janmaat akishangilia vikali bao lake usiku jumatatu kwenye Ligi Kuu England EPL
Bosi wa Chelsea Conte akiwa hoi huku akiwa ameonja machungu ya vipigo viwili
Roberto Pereyra akimchungulia kipa wa Chelsea
Chelsea sasa wako nyuma alama 19 nyuma ya Vinara Manchester City
Eden Hazard alisawazisha bao na kufanya 1-1
Cesar Azpilicueta akipongeza kwa kusawazisha kwenye Uwanja mdogo huo wa Watford Vicarage Road
Straika wa Watford Troy Deeney akishangilia bao lake mbele ya mashabiki huku akiwa amenyoosha kidole cha kati!!
Deeney akishangilia bao lake la mkwaju wa penati huku kipa wa Chelsea akiwa hana hamu!!!!