Tuesday, February 6, 2018

FULL TIME: YANGA 4-0 NJOMBE MJI, CHIRWA APIGA HAT TRICK YANGA IKIIFUNGA MJI NJOMBE 4-0 UWANJA WA UHURU


OBREY Chirwa ameendelea kuing’arisha Yanga baada ya kuifungia mabao matatu katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Njombe Mji kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo ya raundi ya pili ya Ligi Kuu, Yanga ilitawala kila idara hasa katika kipindi cha pili baada ya Njombe kucheza pungufu kutokana na kipa wake Rajabu Mbululo kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kudaka mpira nje ya eneo lake.
Baada ya kwenda mapumziko kila upande ukiwa hauna bao, ilimchukua Chirwa dakika mbili baada ya kipindi cha pili kuiandikia Yanga bao la kuongoza.
Chirwa alifunga bao hilo akiunganisha pasi ya winga ya kulia kutoka kwa Pius Buswita.Dakika ya 65 Chirwa alifunga bao kwa mkwaju wa penalti iliyotolewa na mwamuzi Hance Mabena wa Tanga baada ya beki wa Njombe kuunawa mpira eneo la hatari kabla ya Emmanuel Martin hajaifungia bao la tatu dakika nne baadae akimalizia mpira wa Juma Mahadhi.
Zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya kumalizika kwa mchezo, Chirwa aliandika bao la nne akiunganisha pasi kutoka kwa Baruan Akilimali.
Matokeo hayo yameifanya Yanga kufikisha pointi 34 nyuma ya Azam yenye pointi 31 na Simba yenye pointi 38. Simba inakutana na Azam leo katika mechi yenye presha kubwa kwani kila moja inawania ushindi ili ijisogeze ilipo.