Monday, February 12, 2018

KAMALA CUP 2018 HIYOO YAJA, KUANZA KUTIMUA VUMBI 15/02/2018 KATIKA UWANJA WA KAITABA.


Mh. Diwani Kamala Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo
anawaletea Kitimtim cha Ligi yake ambayo itaanza wiki hii tarehe 15/02/2018 kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.Timu 16 kushiriki Ligi ambayo itashirikisha Vijana kutoka Manispaa ya Bukoba. Hivyo anawaomba Wakazi wa Mji wa Bukoba na Vitongoji vyake kujisogeza kwa Wingi katika Uzinduzi huo utakaofanyika siku ya Alhamisi kuanzia saa 8:00 Mchana. Mtanadao wa www.bukobasports.com utakuletea mbashara Kitimtim hicho kuanzia Ufunguzi huo mpaka tamati.