Monday, February 12, 2018

KITIMTIM CHA LIGI YA KAMALA CUP 2018 KUPIGWA WIKIENDI HII KWENYE UWANJA WA KAITABA MJINI BUKOBA.

Mh. Diwani Kamala Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo anawaletea Kitimtim cha Ligi yake ambayo itaanza wiki hii tarehe 15/02/2018 kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.
Timu 16 kushiriki Ligi ambayo itashirikisha Vijana kutoka Manispaa ya Bukoba. Hivyo anawaomba Wakazi wa Mji wa Bukoba na Vitongoji vyake kujisogeza kwa Wingi katika Uzinduzi huo utakaofanyika siku ya Alhamisi kuanzia saa 8:00 Mchana. Mtanadao wa www.bukobasports.com utakuletea mbashara Kitimtim hicho kuanzia Ufunguzi huo mpaka tamati.