Friday, February 16, 2018

MANE APIGA HAT-TRICK WAKATI LIVERPOOL ILIPOWAFUNGA 5-0 FC PORTO


Sadio Mane amefunga magoli matatu yaani hat-trick wakati Liverpool ikipata ushindi mnono katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuichakaza FC Porto kwa magoli 5-0 kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania kutinga hatua ya 16 bora.
Mane alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu baada ya kipa Jose Sa kushindwa kunyaka mpira wa shuti la Firmino, kisha baadaye Mohamed Salah alionyesha utulivu wake katika ufungaji na kufunga goli la pili. Roberto Firmino alifunga goli la tano.
Sadio Mane akifunga goli la kwanza la Liverpool katika mchezo huo.

Mshambuliaji Mohamed Salah akiifungia Liverpool goli la pili