Thursday, February 1, 2018

MWANAMUZIKI WA UGANDA MOWZEY RADIO AFARIKI DUNIA LEO


Mwanamuziki nyota wa Uganda Moses Ssekibogo, maarufu kama Mowzey Radio, amefariki dunia mmoja wa wanafamilia wa karibu amethibitisha leo asubuhi.
Mmoja wa meneja wake Balaam Barugahara, ameliambia gazeti la New Vision, kuwa Radio amefariki dunia leo majira ya saa 12: 00 alfajiri katika hospitali ya Case Kampala.
 Radio alikuwa amelazwa baada ya kupigwa kwenye baa huko Entebbe wiki mbili zilizopita na kumsababishia majeraha kichwani yaliyopelekea kupasuliwa kichwa kwa matibabu.