Friday, February 16, 2018

RONALDO AWEKA REKODI WAKATI REAL MADRID IKISHINDA BAO 3-1 DHIDI PSG


Magoli mawili ya Cristiano Ronaldo yameisaidia Real Madrid kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Paris St-Germain.
Mshambuliaji huyo raia wa Ureno alifunga goli la pili dakika za mwisho, baada ya hapo awali kufunga goli kwa mkwaju wa penati lililoisawazishia Real Madrid goli lililofungwa na Adrien Rabiot katika nusu ya kwanza.
Beki wa kushoto Mbrazil Marcelo alikamilisha ushindi kwa kufunga goli la tatu dakika tatu tu kupita tangu Ronaldo kufunga goli lililopikwa na Marco Asensio. Ronaldo ameweka rekodi kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 100 UEFA kwa klabu mmoja.


Adrien Rabiot wa PSG akifunga goli la kwanza katika mchezo huo

Mshambuliaji nyota duniani Cristiano Ronaldo akifunga goli lake la pili