Thursday, February 22, 2018

UEFA CHMPIONS LEAGUE: SHAKHTAR DONETSK YAIFUNGA ROMA BAO 2-1.

Shakhtar Donetsk imetokea nyuma na kuifunga Roma magoli 2-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16, shujaa akiwa kiungo kinda Mbrazil Fred.
Mshambuliaji raia wa Argentina, Facundo Ferreyra, aliifungia Donetsk goli la kusawazisha baada ya Roma kuwa wa kwanza kufunga goli kupitia kwa Cengiz Under.
Fred, 24, ambaye amekuwa akihuishwa na kuhamia Ligi Kuu ya Uingereza alifunga kwa shuti la mpira wa adhabu wa kuzungusha uliojaa kwenye kona ya juu ya goli.
Cengiz Under akiifungia Roma goli la kwanza katika mchezo huo
Mpira uliopigwa na kiungo kinda Mbrazil Fred ukijaa wavuni na kuandika goli la pili na la ushindi kwa Shakhtar Donetsk