Sunday, February 4, 2018

VPL:SIMBA YAILAZA RUVU SHOOTING 3-0


SIMBA leo imezidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kuishindilia Ruvu Shooting mabao 3-0 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Kipigo hicho kimeifanya Shooting kuchapwa jumla ya mabao 10-0 msimu huu, baada ya kukubali kufungwa mabao 7-0 katika raundi ya kwanza mwaka jana.
Mabao yaliyofungwa na nahodha John Bocco na Mzamiru Yassin yalitosha kuifanya Simba iendelee kutamba kileleni kusaka ubingwa wa ligi ilioukosa kwa tarkiban miaka mitano.
Bocco anayeonekana kujijengea ufalme Simba baada ya kufanya hivyo Azam misimu kadhaa iliyopita, aliiandikia Simba bao la kuongoza katika dakika ya 22 akiunganisha kona iliyochongwa na Shizza Kichuya.
Katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza, mpira ulilazimika kusimama baada ya kuzimia kwa mshambuliaji mkongwe wa Simba, Emmanuel Okwi aliyefanyiwa madhambi na beki Mau Bofu wa Ruvu ambapo alimpiga shingoni.
Rafu hiyo ilifanya mwamuzi Hance Mabena wa Tanga kumwonyesha kadi nyekundu mchezaji huyo wa Ruvu.


Kutoka na rafu aliyofanyiwa, Okwi hakuendelea na mchezo na hivyo nafasi yake kuchukuliwa na Laudit Mavugo.
Dakika ya 66, Mzamiru aliiandikia Simba bao la pili akiunganisha pasi ya Kichuya kabla Bocco hajaifungia timu yake bao la tatu katika dakika ya 75.
Bocco alifunga bao hilo baada ya kuwavisha kanzu mabeki na kipa wa Ruvu kabla ya kuujaza mpira wavuni. Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha pointi 38 juu ya Azam iliyo nafasi ya pili ikiwa na pointi 33 huku Yanga ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 31. Simba itacheza mechi inayofuata dhidi ya Azam