Wednesday, March 7, 2018

CRISTIANO RONALDO NA CASEMIRO WATUPIA NYAVUNI REAL MADRID IKITINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA DHIDI YA PSG


Cristian  Ronaldo

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Real Madrid wametinga katika hatua ya robo fainali wakiifunga Paris St-Germain kwa magoli 2-1 katika dimba la Parc des Princes.
Cristiano Ronaldo aliyefunga magoli mawili katika mchezo wa kwanza wakiibuka na ushindi wa magoli 3-1, alifunga goli la mpira wa kichwa kufuatia krosi ya Lucas Vazquez.
PSG ilijikuta kiungo wake Marco Verratti akitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kucheza rafu kabla ya Edinson Cavani kusawazisha goli, lakini Casemiro akafunga goli la pili.


Cristiano Ronaldo akiwa ameruka juu na kuupiga mpira kwa kichwa na kufunga goli

Casemiro akifunga goli la pili la Real Madrid na kufanya matokeo kuwa 2-1