Wednesday, March 7, 2018

KLOPP AJIGAMBA KUTINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAY, ATOKA 0-0 NA FC PORTO USIKU

Kocha Jurgen Klopp amesema Liverpool inastahili kuwa katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutoa sare ya 0-0 dhidi ya Porto, na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa magoli 5-0.
Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 2009 kwa Liverpool kutinga hatua hiyo, lakini kocha Klopp amesisitiza kuwa hili si suala la miujiza mikubwa.
Timu ya Liverpool ilishinda magoli 5-0 nchini Ureno katika mchezo wa awali na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga katika mchezo wa jana nyumbani Anfield.
Kipa wa Liverpool Loris Karius akidaka mpira uliopigwa na Majeed Waris
Mohamed Salah akisikitika baada ya mpira aliopiga kuzuiliwa na kipa Iker Casillas