Tuesday, March 6, 2018

MAN CITY YAPIGA PASI NYINGI WAKIITUNGUA 1-0 CHELSEA, ARSENAL NAYO YANYUKWA BAO 2-1

Kocha wa Chelsea Antonio Conte ametetea mbinu zake za mchezo licha ya kulala kwa goli moja kwa bila dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Manchester City.
Chelsea ilionyesha mpira wa kujihami mno kiasi ya kutopiga shuti lililolenga goli la wapinzani wao, na kujikuta wakilala kwa goli lililofungwa na Bernardo Silva.


Bernardo Silva akiuwahi mpira na kufunga goli pekee katika mchezo huo

Brighton imeifunga Arsenal kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1982 na kuongeza shinikizo la kutaka kutimuliwa kocha Arsene Wenger.
Lewis Dunk aliifungia Brighton goli la kwanza na kisha baadaye Glenn Murray akaongeza goli la pili huku Pierre-Emerick Aubameyang akiifungia Arsenal goli la kufutia machozi.


Glenn Murray akifunga goli la pili la Brighton kwa mpira uliomshinda kipa Petr Cech