Sunday, March 18, 2018

MANCHESTER UNITED YAIFUNGA BRIGHTON NA KUTINGA NUSU FAINALI FA


Mshambuliaji nyota Romelu Lukaku amefunga goli lake la 12 katika michezo 11 ya Kombe la FA, wakati Manchester United ikiifunga Brighton magoli 2-0 na kutinga nusu fainali ya kombe hilo.
Lukaku alifunga goli la kwanza kwa kichwa akiunganisha krosi ya Nemanja Matic, ambaye alifunga goli la ushindi la dakika za mwisho kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Ashley Young.


Ushindi huo unaongeza matumaini ya Manchester United kutwaa kombe hilo baada ya kutolewa Ligi ya Mabingwa Ulaya jumanne na Sevilla, huku wakiendeleza rekodi ya kutofungwa goli katika michuano ya FA msimu huu.

Mshambuliaji nyota wa Manchester United Romelu Lukaku akifunga goli la kwanza kwa mpira wa kichwa

Kiungo mkabaji Nemanja Matic akifunga goli la pili la Manchester United