Tuesday, March 6, 2018

MANCHESTER UNITED YATOKA NYUMBA NA KUILIMA BAO 3-2 CRYSTAL PALACE KWAO!


Nemanja Matic amefunga goli tamu la dakika ya mwisho na kuipatia ushindi Manchester United iliyokuwa nyuma kwa magoli 2-0 na kukwea hadi nafasi ya pili ya msimamo wa ligi.
Manchester United ilijikuta ikifungwa goli la kwanza katika kipindi cha kwanza na Andros Townsend na kisha Patrick van Aanholt akaongeza la pili katika kipindi cha pili.
Hata hivyo beki Chris Smalling akafunga goli la kwanza la Manchester United kwa kichwa kisha Romelu Lukaku akafunga la pili na Matic la tatu na matokeo kuwa 3-2.


Romelu Lukaku akifunga goli la pili la Manchester United

Kiungo mkabaji Nemanja Matic akichia shuti kali lililozaa goli la tatu