Wednesday, March 14, 2018

MARCUS RASHFORD AIZAMISHA LIVERPOOL OLD TRAFFORD, ATUPIA BAO MBILI FASTA NDANI YA DAKIKA 25.


Marcus Rashford amefunga magoli mawili wakati Manchester United ikifanikiwa kuituliza Liverpool kwa kuifunga magoli 2-1 na kuendelea kung'ang'ani katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi.
Matokeo hayo yanakifanya kikosi hicho cha Jose Mourinho kupunguza pengo na vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Manchester City kuwa pointi 13 hadi hapo City itakapocheza na Stoke jumatatu.
Rashford, ambaye alianza mchezo huo kwa mara ya kwanza tangu Desemba 26, atapamba vichwa vya habari lakini Romelu Lukaku ndiye alikuwa chachu ya kupatikana kwa magoli hayo kutokana na Liverpool kushindwa kudhibiti maguvu yake.


Marcus Rashford akiangalia mpira ukielekea langoni mwa Liverpool baada ya kuachia shuti lililozaa goli la pili

Kipa David De Gea akishindwa kuzuia mpira wa goli la kujifunga uliopigwa na beki Eric Bailly