Tuesday, March 6, 2018

RONALDO NA BALE WAIONGOZA REAL MADRID KUPATA USHINDI WA BAO 3-1


Cristiano Ronaldo amefunga mara mbili wakati Real Madrid ikirejesha makali yake ya ushindi kwa kuwafunga Getafe waliobakia 10 uwanjani katika mchezo wa La Liga .
Kikosi hicho cha Zinedine Zidane kilichofungwa na Espanyol jumanne, lakini katika mchezo wa jana Gareth Bale alikuwa wa kwanza kufunga goli la kuongoza dhidi ya Getafe.
Ronaldo alifunga goli lake la kwa kwa shuti la chini likiwa goli lake la 300 La Liga, kabla ya kufunga goli lake la pili kwa mpira wa kichwa dakika ya 78, na matokeo kuwa 3-1.


Mshambuliaji Gareth Bale akifunga goli la kwanza la Real Madrid

Cristiano Ronaldo akiwa ameruka juu na kufunga kwa mpira wa kichwa goli la tatu