Friday, March 2, 2018

TIMU YA MANCHESTER CITY YAICHAPA TENA ARSENAL 3-0

Manchester City imeonyesha kiwango bora zaidi na kuichapa kwa mara ya pili Arsenal kwa magoli 3-0 na kuongeza uongozi wao wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa tofauti ya pointi 16.
Kwa matokeo hayo Manchester City inahitaji kushinda michezo mitano tu ili kuwa bingwa huku ikiwa imebakiza michezo 10 katika ligi hiyo.
Baada ya kuichapa Arsenal magoli 3-0 katika kombe la Carabao jumapili, Manchester City ilipata goli la kwanza kupitia kwa Bernardo Silva ndani ya dakika 15.
Silva akaongeza goli la pili katika dakika ya 28, kabla ya baadaye Leroy Sane kufunga goli la tatu lililoimaliza kabisa Arsenal.
Bernardo Silva akifunga goli baada ya kuwazidi maarifa walinzi wa Arsenal
Leroy Sane akikamilisha kipigo cha Arsenal kwa kupachika wavuni goli la tatu
Kocha Arsene Wenger akisikilizia maumivu ya kipigo kwa kuinama huku akishikilia kichwa