Wednesday, April 11, 2018

BARCELONA YATOLEWA NJE LIGI YA MABINGWA ULAYA


Roma imewabadilikia Barcelona katika mchezo wao wa marudio kwa kutandaza soka safi na kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 na kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa goli walilofunga ugenini katika mchezo wa kwanza.
Barcelona walikuwa wakipewa kipaumbele cha kutinga nusu fainali baada ya ushindi wa magoli 4-1 katika mchezo wa kwanza, lakini jana walijikuta wakigonga mwamba kufuatia Roma kuonyesha uerevu wa hali ya juu.

Beki Kostas Manolas alifunga goli muhimu la tatu kwa mpira wa kichwa kwenye kona ya goli zikiwa zimebakia dakika nane mpira kuisha. Edin Dzeko alifunga goli la kwanza la mapema na Daniele de Rossi akaongeza la pili kwa mkwaju wa penati.

Beki Kostas Manolas akifunga kwa kichwa la tatu lililoitoa Barcelona UEFA

Kapteni Lionel Messi akiwa ameinamisha kichwa chini baada ya Barcelona kutolewa UEFA