Monday, April 16, 2018

JAPHARY KIBAYA AINYAMAZISHA MTIBWA KAITABA KWENYE DEBI YAO YA SUKARI KWA KICHAPO CHA BAO 2-1

Mgeni Rasmi wa Mchezo huo wa VPL kati ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar akiwasilimia Waamuzi wa Mtanange huo muda mfupi kabla ya mchezo kuanza. 

Na Faustine Ruta, Bukoba
Katika Mchezo huo ulianza kwa kasi sana Timu ya Mtibwa Sugar ndio ilianza kuliandama lango la Timu ya Kagera Sugar na kufanikiwa kupata bao la kwanza kupitia kwa Mchezaji wake Salum Kiimbwa aliyeunganisha kwa kichwa mpira nyavuni baada ya kupokea krosi mapema kipindi cha kwanza dakika ya 26. Kagera Sugar nao waliongeza kasi na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 45 kupitia kwa mshambuliaji wake Japhary Kibaya aliyewatoka mabeki wa Mtibwa na kuiwezesha kwenda mapumziko kwa bao 1-1. Kipindi cha pili Kagera Sugar walifanya mabadiliko kwa Wachezaji na kuweza kuongeza kasi kubwa na kuweza kupata bao tena la pili kupitia kwa mchezaji huyo huyo Japhary Kibaya aliyeunganisha mpira kwa kichwa na kufanikiwa kuwapa bao la pili Kagera Sugar na kuweza kuibuka Kidedea cha bao 2-1 dhidi ya Timu ya Mtibwa Sugar. Hadi Dakika 90 zinakamilika Kagera Sugar 2-1 mtibwa Sugar.
Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar  kilichoanza dhidi ya Timu ya Mtibwa Sugar  leo
Kikosi cha Timu yaMtibwa Sugar kilichoanza dhidi ya Kagera Sugar leo kwenye Mchezo wa Ligi Kuu Bara VPL.
Picha zote na Faustine Ruta, Bukoba
Picha Ya Pamoja Manahodha Timu zote mbili na Waamuzi
Mecky Maxime akisalimiana na Kiongozi wa  Mtibwa Sugar
Viongozi pande zote mbili Mecky Maxime na kiongozi wa Mtibwa Sugar wakiteta jambo kwa furaha walipokutana Kaitaba kwenye Mchezo wao wa Dabi ya Miwa ukiwa ni Mchezo wa Ligi Kuu Bara VPL.

Sehemu ya Benchi la Timu ya Mtibwa Sugar(kulia) niShaaban Hassan Kado.
Japhet wa Kagera Sugar akigombea mpira dhidi ya mchezaji wa Mtibwa Sugar.


Kibaya tena ....akijisimamia na mpira...
kulia ni Mchezaji wa Kagera Sugar Japhary Kibaya akiendesha mpira kumtoka mchezaji wa Mtibwa Sugar.

Mchezaji wa Kagera sugar Japhet akimtoka mchezaji wa Mtibwa Sugar leo hii kwenye Mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba, Kagera Sugar ameifunga Timu ya Mtibwa Sugar bao 2-1.Baadhi ya Wachezaji wa Kagera Sugar wakimpongeza Mchezaji mwenzao Japhary Kibaya mara baada ya kuwafungia bao la pili na kufanya matokeo kuwa 2-1 katika kipindi cha pili baada ya kwenda mapumziko kwa bao 1-1.
Picha zote na Faustine ruta, Bukoba
Baadhi ya Wachezaji wa Kagera Sugar wakimpongeza Mchezaji mwenzao Japhary Kibaya mara baada ya kuwafungia bao la pili na kufanya matokeo kuwa 2-1 katika kipindi cha pili dakika ya 53.
Mwamuzi akiwarudisha wachezaji wa Kagera Sugar Uwanjani kuendelea na mchezo..
Kocha wa Timu ya Kagera Sugar, Mecky Maxime, Picha zote na Faustine Ruta, Bukoba
Sehemu ya Benchi la Timu ya Kagera Sugar.

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar Zuberi Katwila akishangaa mara baada ya Timu yake kufungwa bao la pili, Na Matokeo kuwa 2-1.
Japhary Kibaya(kulia) leo ndiye aliyewapa Ushindi Kagera sugar kwenye Dabi yao dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mchezaji wa Kgaera Sugar aliyevaa jezi namba 13 maarufu kama Kagawa akipanga kuwatoka Mabeki wa Timu ya Mtibwa Sugar.
Mpira ni furaha!!.....Meneja wa Kagera Sugar Mecky Mexime akiteta jambo na Mchezaji wa Mtibwa Sugar leo wakati wa mchezo wao.  Ukumbuke pia mpenzi msomaji wetu wa bukobasports.com,  Mecky Mexime alikuwa Kocha wa zamani wa timu hiyo ya Mtibwa Sugar zamani ambayo ina Makazi yake Mjini Morogoro.
Kagawa Tena akiendesha mpira
Wakati mpira ulipomalizika Mecky Maxime aliwatembelea Wachezaji wa Timu ya Mtibwa Sugar kwenye Gari lao.
Picha zote na Faustine Ruta, Bukoba
Wachezaji wa Timu ya Kagera Sugar wakifurahia Ushindi wao dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Basi lao mara baada ya mtanange huo kumalizika.
Kagera Sugar....Mambo safi leo!!! Thumb up!!
Shangwe Kwa Kagera Sugar. Kagera sugar imeifunga Timu ya Mtibwa Sugar bao 2-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Picha zote na Faustine Ruta, Bukoba