Wednesday, April 11, 2018

LIVERPOOL YAIZAMISHA TENA MANCHESTER CITY UEFA, KWA BAO 2-1, KLOPP ACHEKELEA..!


Timu ya Liverpool imetinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu kupita miaka 10 baada ya kutokea nyuma kufungwa goli moja na kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Manchester City.
Wenyeji Manchester City walianza vizuri kwa kumiliki mpira tangu mwanzo wakijaribu kubadili matokeo ya mchezo uliopita ya kufungwa magoli 3-0 na alikuwa Gabriel Jesus aliyefunga goli la kwanza.

Liverpool ilichomoa goli hilo katika kipindi cha pili kupitia kwa Mohamed Salah mnamo dakika ya 56, kufuatia pasi ya kutanguliziwa na Sadio Mane kisha baadaye zikiwa zimesalia dakika 13 Roberto Firmino akaongeza la pili.

Mohamed Salah akifunga goli la kusawazisha lililochangia kubadilisha mchezo

Kocha Jurgen Klopp akipiga ngumi hewa kushangilia goli alilofunga Mohamed Salah