Monday, April 2, 2018

NGORONGORO HEROES YAMPA RAHA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

TIMU ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania, Ngorongoro Heroes, imetoa zawadi kwa Watanzania baada ya kuifunga Morocco 1-0 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Bao hilo pekee lililoitoa kifua mbele Ngorongoro Heroes, lilifungwa na Muksin Makame katika dakika ya 73 kwa penalti baada ya mlinzi wa Morocco Limourt Youssef kuunawa mpira katika eneo la hatari.


Katika mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki, timu hizo zilicheza kwa kushambuliana kwa zamu, huku zikitoa burudani safi kwa watazamaji walioingia bure uwanjani.
Baada ya mchezo huo, Ngorongoro Heroes Jumatano watacheza dhidi ya Msumbiji katika mchezo mwingine wa kirafiki kujiandaa na mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Pamoja na kuwa ni mchezo wa kirafiki, lakini ushindi huo ni muhimu kwa Ngorongoro kwani timu za Tanzania kuanzia zile za klabu na taifa zimeshindwa kabisa kuzifunga timu za Morocco. Kikosi cha Ngonrongoro: Aboutnalib Msheli, Kibwana Shomary, Nickson Kibabage, Ally Msengi, Dickson Job, Ally Ngazi, Hassadi Juma, Kelvin Naftal, Maziku Aman, Abdul Seleiman na Said Bakari.